From Wikipedia, the free encyclopedia
Bongo Flava ni jina badala la muziki wa Hip hop ya Tanzania. Mtindo huu ulianzishwa kwenye miaka ya 1990, hasa ukiwa kama mwigo au utokanaji wa hip hop kutoka Marekani, ikiwa na ongezeko la athira ya muziki wa reggae, R&B, afrobeat, dancehall, na mitindo ya asili ya Kitanzania kama vile taarab na dansi, muunganiko ambao umeunda mtindo wa pekee wa muziki.[1] Mashairi kwa kawaida huwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
Makala hii, au sehemu za makala hii, inahitaji vyanzo au marejeo yoyote. Tafadhali saidia kuboresha makala hii kwa kuweka vyanzo vya kuaminika. Habari zisizowekewa vyanzo zinaweza kuwekewa alama na kuondolewa. (May 2014) |
Bongo Flava | |
---|---|
Asili ya mtindo | Hip hop, Tanzanian music |
Asili ya utamaduni | 1990s Tanzania |
Ala | Bass guitar, drums, guitar, keyboards, percussion, vocals |
Inapotendeka | |
Dar es Salaam |
Jina la "Bongo Flava" ni tokeo la matini yaliyoharibiwa kutoka "bongo flavour", ambapo "bongo" ni wingi wa neno ubongo, ambapo mara nyingi huchukua nafasi ya kutaja jina la utani la Dar es Salaam, jiji ambalo aina ya mtindo huu inatokea na wakati mwingine humaanisha pia nchi ya Tanzania. Katika bongo flava, sitiari ya "bongo" inaweza kutaja zaidi maana ya ujanjaujanja wa mtaani, ya msela au masela wingi wake.[2]
Istilahi ya "Bongo Flava" ilitajwa kwa mara ya kwanza mnamo 1996 na Radio One 99.6 FM (moja kati ya redio za kwanza kabisa za binafsi nchini Tanzania) DR wa Redio Mike Mhagama ambaye alikuwa akijaribu kutofautisha kati ya muziki wa R & B na hip hop wa Marekani kupitia lipindi chake maarufu cha redio - 'DJ Show' ambapo enzi hizo vijana chipukizi walikuwa hawajaanza kutamba kwa mitindo yao wenyewe. DJ Show kilikuwa kipindi cha kwanza cha redio kukubali wanamuziki vijana wa Kitanzania wenye athira ya muziki wa Marekani - wakijieleza wenyewe kupitia uimbaji wa rap. Alisema hewani, "Baada ya kusikiliza kibao cha "R & B Flava" kilichoitwa 'No Diggity' kutoka Marekani, sasa inakuja "Bongo Flava" kutoka kwa Unique Sisters, kutoka hapa nyumbani." Baada ya kusema hivyo katika kipindi, istilahi hii ya "Bongo Flava" ikanasa hadi leo hii.
Asili ya mwanzo kabisa na jinsi "Bongo flava" ilivyoanzishwa nchini Tanzania ni kutokana na Taji Liundi akiwa kama kiini cha hadithi hii. Kifupi hakuna asili bila yeye. Taji Liundi pia anajulikana kama Master T, mwasisi, mwanzilishi na vilevile mtayarishaji wa kipindi cha Dj Show alishaanza kupiga nyimbo za wasanii wa ndani tangu mwishoni mwa miaka ya 1994. Mike Mhagama baadaye akajiunga na kipindi akiwa chini ya ukufunzi wa Master T. Aliendelea na kutangaza kipindi hicho peke yake hata baada ya Master T kuondoka Radio One mnamo 1996.
"Bongo Flava" ilikaa vizuri sana hata kabla ya rekodi za video au sauti. Vijana mjini Dar es salaam walikuwa wakirap ufukweni mwa bahari kupitia matamasha mbalimbali (yameandaliwa na Joseph Kusaga ambaye anamiliki Mawingu Discothèque, baadaye Mawingu Studios na sasa ni Clouds Media Group), matamasha ya ndani yaliyochukua sura mpya rasmi baada ya kuanzisha mfululozo wa shindano la Yo!Rap Bonanza ambalo lilikuwa likichochewa na DJ Kim "And the Boyz" Magomelo.
Baadhi ya vijana walikuwa wakijipanga au kujiita majina ya kutunga au kundi fulani, baadhi yao walikuwa wakijitegemea au kujiweka katika kikundi fulani katika tukio hilo ilimradi wapate nafasi ya kukamata mic. Moja kati ya waliowahi kutamba katika mashindano ya kushika mic mwanzoni mwa miaka ya 1990 ni pamoja na Adili au Nigga One. Msanii maarufu wa kwanza wa mtindo huu aliyewahi kuiga ngoma za Marekani ni Saleh Jabir ambaye alirap kwa Kiswahili kupitia biti ya Vanilla Ice, "Ice Ice Baby", yeye ndiye aliyeanza kuweka Kiswahili katika rap. Toleo lake lilikuwa maarufu, ilivunja rekodi na kuweza kupigwa hata katika Redio ya Taifa la Tanzania. Ulikuwa wimbo wa kwanza wa rap ya Kiswahili kupaa anga ya Tanzania.
Moja kati ya makundi ya mwanzo kabisa kurekodi na kupeleka CD Radio One ili irushwe ilikuwa bendi ya Mawingu, kundi ambalo lilitamba sana mwanzoni mwa miaka ya 1994. Walirekodia katika Studio za Mawingu. Wanachama wake walikuwa kina Othman Njaidi, Eliudi Pemba, Columba Mwingira, Sindila Assey, Angela, Robert Chuwa, Boniface Kilosa (a.k.a. Dj Boni Love) na baadaye Pamela ambaye aliimba kibao chao kilichovunja rekodi cha RnB/Rap "Oya Msela". Wimbo ulikuwa maarufu mno na baadaye hilo neno likabaki hadi leo. Bendi ya Mawingu hujadilika kama waanzilishi wa ladha aina ya RnB ya Bongo flava. Dar Young Mob lilikuwa kundi la kwanza la hip hop ya kweli kurekodi na Mawingu Studios chini ya utayarishaji wake Dj Boni Love. Lilikuwa kundi la kwanza kupigiwa kibao chao katika redio ya binafsi nchini Tanzania.
Kundi la kwanza la hip hop la Tanzania, Kwanza Unit, 1993. Awali walikuwa wanaimba kwa Kiingereza lakini hatimaye wakawa wanaimba kwa Kiswahili. Moja kati ya wanachama wa zamani wa kundi hili ni Professor Jay, kwa ni moja kati ya wasanii maarufu wa hip hop nchini Tanzania. Vilevile kundi la Diplomate lililokuwa na kina Saigon.
Miongoni mwa wasanii maarufu wa Bongo Flava kwa sasa ni pamoja na Ali Kiba, Juma Nature, Lady Jaydee, Mzungu Kichaa, Geezy Mabovu, Q Chillah, TID, Diamond Platnumz, Dknob na wasanii wapya wa Bongo Flava kama vile Nay wa Mitego, Ben Pol, Dogo Fani na wengine wengi kama Gangwe Mobb, Dully Sykes na Daz Baba.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.