Tambarare ya Uhindi Kaskazini ni eneo kubwa la bara upande wa kusini wa Milima ya Himalaya linaloshika Uhindi Kaskazini yote na Bangladesh yote pamoja na sehemu za Pakistan na Nepal.

Thumb
Maeneo ya tambarare ya Uhindi Kaskazini.
Thumb
Mashariki mwa tambarare (India, Bangladesh na Nepal) kwa macho ya satelaiti; Mto Ganges uko katikati ya tambarare.

Tambarare hiyo imesababishwa na mito miwili ya Indus na Ganges na ina kilomita za mraba milioni 2.5[1]. Inakaliwa na watu bilioni 1 yaani sehemu ya saba ya watu wote duniani.

Tambarare yote imegawiwa katika mabeseni ya mito miwili: maji upande wa magharibi huelekea mto Indus na upande wa mashariki huelekea mto Ganges.

Tambarare hiyo inapokea maji yake kutoka milima ya Himalaya hasa; mito hiyo imetelemka pamoja na matope yaliyojenga tabaka nene la ardhi yenye rutuba. Hivyo ni eneo linalofaa kwa kilimo hasa cha mpunga na ngano kinacholisha idadi kubwa ya watu.

Katika historia ya binadamu ilikuwa kati ya maeneo ya kwanza ambako milki na utamaduni wa miji vilianzishwa vikiwezesha kuwepo kwa wataalamu walioweka misingi ya sanaa na elimu ya juu.[2]

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.