From Wikipedia, the free encyclopedia
Historia ya Ufini inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Ufini.
Ufini ulikaliwa na watu tangu ilipokwisha enzi ya barafu ya mwisho, miaka 9000 KK hivi.[1] Wakazi wa kwanza walikuwa wawindaji-wakusanyaji ambao walitumia vifaa vya mawe vinavyofanana na vile vya Estonia, Russia na Norway.
Mwishoni mwa karne ya 13 Ufini ukawa sehemu ya Sweden hadi mwaka 1809, ilipomezwa na Dola la Russia kama ufalme mdogo wenye kujitawala kwa kiasi fulani.
Mwaka 1906, Ufini ulikuwa nchi ya kwanza duniani kuwapa wananchi wote wenye umri wa utu uzima haki ya kugombea vyeo vya serikali.[3][4]
Mwaka 1917, baada ya Mapinduzi ya Russia, Ufini ulijitangaza huru na mwaka uliofuata ukawa jamhuri baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wakati wa vita vikuu vya pili, Muungano wa Kisovyeti ulijitahidi kuteka Ufini wote, ukaishia kutwaa Karelia, Salla, Kuusamo, Petsamo na visiwa kadhaa tu.
Baada ya vita Ufini uliacha kutegemea kilimo ukajitosa katika uchumi wa viwanda[5] hata kufikia kuwa kati ya nchi zilizoendelea zaidi[6][7][8][9][10][11][12].
Mwaka 1955 Ufini ulijiunga na Umoja wa Mataifa ukichagua siasa ya kutoambatana na upande wowote.
Mwaka 1995 ulijiunga na Umoja wa Ulaya na mwaka 1999 ulikubali kutumia euro.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.