From Wikipedia, the free encyclopedia
Hati ya Damasi (au De explanatione fidei) ilitolewa na Papa Damasus I mwaka 382[1].
Kwa hati hiyo alithibitisha orodha rasmi ya vitabu vya Biblia ya Kikristo katika Kanisa Katoliki.
Orodha hiyo ilipata nguvu Afrika Kaskazini kutokana na Agostino wa Hippo kuifanya ipitishwe na Mtaguso wa Hippo (393), Mtaguso wa tatu wa Kartago (397) na Mtaguso wa nne wa Kartago (419).
Wakati huohuo Papa Inosenti I aliituma kwa askofu Esuperi wa Toulouse (405).
Baadaye Mtaguso wa Firenze (1442) na Mtaguso wa Trento (1546) ilivitambua rasmi kuwa sehemu za Biblia kamili kwa Kanisa Katoliki.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.