From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Damaso I (takriban 304 – 11 Desemba 384) alikuwa Papa kuanzia tarehe 1 Oktoba 366 hadi kifo chake[1]. Alitokea Roma, Italia. Jina lake la kuzaliwa pia lilikuwa Damasus.
Alimfuata Papa Liberius akafuatwa na Papa Siricius.
Mchango wake mkubwa zaidi ni kuthibitisha kanuni ya Biblia kama ilivyo hadi leo katika Kanisa Katoliki.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni 11 Desemba.[2].
Vitabu vya Deuterokanoni vilihesabiwa rasmi kuwa sehemu ya Biblia hasa kuanzia Hati ya Damasi au De explanatione fidei, iliyotolewa na Papa Damasus I mwaka 382 (kwa Kilatini).
Tafsiri ya Kilatini ya Hieronimo kilichoitwa Vulgata ilipata kuwa toleo muhimu katika Kanisa Katoliki hadi leo. Hieronimo mwenyewe alipotafsiri Biblia upya katika Kilatini alisema vitabu vya Septuaginta kama Kitabu cha Hekima, Kitabu cha Yoshua bin Sira, Kitabu cha Yudith na Kitabu cha Tobiti havistahili kuwemo katika Biblia lakini alivitafsiri ndani ya Vulgata kufuatana na maelekezo wa Papa Damaso I aliyemuagiza kazi.[3]
Orodha hiyo ya Papa Damaso I ilipata nguvu Afrika Kaskazini kutokana na Agostino wa Hippo kuifanya ipitishwe na Mtaguso wa Hippo (393), Mtaguso wa Tatu wa Kartago (397) na Mtaguso wa Nne wa Kartago (419).
Wakati huohuo Papa Inosenti I aliituma kwa askofu Exuperius wa Toulouse (405).
Baadaye Mtaguso wa Firenze (1442) na Mtaguso wa Trento (1546) ilivitambua rasmi kuwa sehemu za Biblia kamili kwa Kanisa Katoliki.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.