Papa Liberius
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Liberius alikuwa Papa kuanzia tarehe 17 Mei 352 hadi kifo chake tarehe 24 Septemba 366[1]. Alitokea Roma, Italia.

Alimfuata Papa Julius I akafuatwa na Papa Damaso I.
Alidhulumiwa na kaisari Konstans II, mtetezi wa Uario.
Liberius ni Papa wa kwanza ambaye haheshimiwi na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Hata hivyo Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki wanampa heshima hiyo.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Agosti[2] au nyingine[3].
Maoni chanya ya Mapapa juu yake
- Papa Pius IX katika hati Quartus Supra aliandika kwamba Liberius alisingiziwa tu na Waario, kumbe alikataa kumlaani Atanasi wa Aleksandria. [4]
- Papa Benedikto XV katika hati Principi Apostolorum Petro aliandika kwamba Liberius alikubali hata kupelekwa uhamishoni ili atetee imani sahihi ya Kanisa. [5]
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.