wa thelatini ya nane kitabu Biblia na zingatia kitabu Agano la Kale, mchanganyiko 14 sura ya From Wikipedia, the free encyclopedia
Kitabu cha Zekaria ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh, yaani Biblia ya Kiebrania. Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Kazi ya nabii huyo kati ya mwaka 520 na 518 KK, wakati uleule alipotabiri nabii Hagai, ni mwanzo wa kipindi cha mwisho cha unabii katika Israeli kabla ya ujio wa Yohane Mbatizaji na Yesu Kristo.
Kabla ya uhamisho wa Babeli, ujumbe wa manabii ulitishia mara nyingi adhabu ya Mungu kwa uasi wa taifa lake.
Wakati wa uhamisho ujumbe ulikuwa wa faraja zaidi.
Ule wa Hagai na Zekaria ulilenga ustawi wa Wayahudi ambao walikuwa wamerudi Yerusalemu mwaka 538 KK ili kujenga upya hekalu, lakini walichelewa kutekeleza azma yao, kutokana na upinzani na mahangaiko ya kujipatia riziki katika mazingira magumu.
Mbaya zaidi, walikaribia kukata tamaa. Kwa changamoto ya manabii wao, gavana Zerubabeli na kuhani mkuu Yoshua waliongoza wananchi kukazania ujenzi huo na kuukamilisha mwaka 515 KK.
Kitabu kina sehemu mbili tofauti sana, yaani sura 1-8 halafu 9-14.
Sura nane za kwanza zinaleta njozi kadhaa kuhusu mwanzo mpya wa Wayahudi mjini Yerusalemu.
Tofauti na Hagai, mwandishi wa kitabu hiki hakuishia upande wa ujenzi, bali alisisitiza pia utakaso wa waamini na ibada zao.
Sura nyingine sita zinatokana na mazingira tofauti (ya karne ya 4 KK) na kuleta njozi juu ya ujio wa Masiya na siku za mwisho.
Sura hizo zina mtindo wa kiapokaliptiko na wataalamu wengi wanasema ni kazi ya nabii mwingine wanayemuita Zekaria wa pili.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.