From Wikipedia, the free encyclopedia
Epifani wa Salamina (kwa Kigiriki: Ἐπιφάνιος; Besanduk, karibu na Eleutheropolis, leo Beit Guvrin, Israeli [1]310–320 hivi – 403) alikuwa mmonaki nchini Misri, halafu askofu wa Salamina, Kupro, maarufu kwa juhudi za kutetea imani sahihi ya Kanisa Katoliki[2].
Mwenye elimu kubwa na ujuzi wa maandiko ya Kikristo, msemaji wa lugha tano tofauti[3], anajulikana hasa kwa kitabu chake Panarion alichokitunga miaka 374-377 kwa ajili ya kupinga aina 80 za uzushi zilizoenea kati ya Wakristo[4].
Pamoja na hayo, aling'aa pia kwa maisha matakatifu, ukarimu kwa maskini na karama ya kufanya miujiza.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na Baba wa Kanisa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.