Utakatifu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Utakatifu

Utakatifu (kutoka kitenzi "kutakata") ni ule usafi wa pekee wa Mwenyezi Mungu mwenyewe asiye na mawaa.

Thumb
Qodeš l-Yahweh, "Mtakatifu kwa Yahweh", mwandiko uliovaliwa na kuhani mkuu katika paji la uso.

Kwa binadamu ni hali ya ukamilifu katika kuepukana na dhambi, na hivyo kuwa karibu na Mungu.

Katika Biblia

Neno la Kiebrania Qadosh linamhusu kwa namna ya pekee Mungu katika ukuu wake usioweza hata kufafanishwa na ule wa viumbe vyake bora[1] na unaodai yale yanayomhusu yasichanganywe na matumizi mengine[2].

Katika Kigiriki kuna neno Agios likimaanisha kutokuwa na makosa au udhaifu au uchafu[3].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.