From Wikipedia, the free encyclopedia
Eric Lynn Wright (7 Septemba 1964 – 26 Machi 1995) alikuwa rapa na mtayarishaji wa muziki kutoka mjini Compton, California, Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Eazy-E. Wakati Eazy E bado yungali bwana mdogo alikuwa akijishughulisha na maswala ya uuzaji wa dawa za kulevya, kisha pesa za kazi hiyo anawekeza katika mradi wake wa muziki wa hip hop.
Eazy-E | |
---|---|
Eazy-E mnamo 1993 | |
Taarifa za awali | |
Jina la kuzaliwa | Eric Lynn Wright |
Amezaliwa | Compton, California, U.S. | Septemba 7, 1964
Amekufa | 26 Machi 1995 (umri 30) Los Angeles, California, U.S. |
Kazi yake | Rapper, CEO, mtayarishaji wa rekodi |
Miaka ya kazi | 1986–1995 |
Studio | Ruthless, Priority, Relativity, Epic, MCA |
Ameshirikiana na | N.W.A, DJ Yella, Dr. Dre, The D.O.C., Rhythum D, Above the Law, B.G. Knocc Out & Dresta, Bone Thugs-n-Harmony, Sylk-E. Fyne, Ice Cube, Brownside |
Anafikirika sana kuwa yeye ni mmoja kati ya waanzilishi wakubwa wa kundi la muziki wa hip hip maarufu kama N.W.A., lakini baadaye alipata umaarufu zaidi pale alipokuwa akifanya muziki huo akiwa kama msanii wa kujitegemea (solo artist).
Sauti ya Eazy-E ilikuwa ikijulikana kwakuwa alikuwa akiitumia kwa staili moja tu, alikuwa akiimba kwa sauti ya juu na mashairi yake yalikuwa yakilenga sana maisha ya mtaani, yaani ujambazi, madawa ya kulevya, mahusiano ya wakazi na polisi, na masuala ya kujamiiana.
Kuna kipindi pia alikuwa akitangaza kipindi cha hip hop katika radio ya Los Angeles katika kituo cha KKBT.[1]
Kwa kazi zake za uuzaji wa dawa za kulevya, zilikuwa zikimpa faida sana na akaamua kutumia faida zake kwa kuanzisha studio ya kurekodia mzuiki huo. Studio ilikwenda kwa jina la Ruthless Records.[1] Pale Ruthless ilipo msajiri Dr. Dre na Ice Cube wakatunga nyimbo ya "Boyz-n-the-Hood", kisha Wright akaanzisha kundi liliokwenda kwa jina la N.W.A, kundi likaunganisha marapa wengi kama Dr. Dre na Ice Cube kisha baadaye akaongezeka DJ Yella na Arabian Prince. Baadaye studio ya Ruthless ikatoa albamu ya kwanza ya N.W.A (1987), N.W.A na mwaka uliofuata wakatoa Straight Outta Compton (1988), na baada ya mwezi mmoja Eazy-E akatoa albamu yake binafsi iliyokwenda kwa jina la Eazy-Duz-It.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.