From Wikipedia, the free encyclopedia
Bujugo ni kata ya Wilaya ya Bukoba Vijijini katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35207 [1].
Kata ya Bujugo ni muungano wa vijiji vitatu ambavyo ni: Katoju, Buganguzi na Minazi. Makao makuu yako katika kitongoji cha Bituntu.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 8,102 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,140 waishio humo.[3]
Wakazi wengi wa Bujugo ni Wahaya.
Kata ya Bujugo ina shule ya sekondari moja, ambayo ni Bujugo sekondari, na shule za msingi nne ambazo ni: Bujugo, Minazi, Lutimbiro na Katoju.
Shughuli za kiuchumi ni kilimo cha mazao ya chakula kama ndizi, mihogo, viazi, mahindi, maharagwe, karanga, njugu mawe n.k. Pia kuna mazao ya biashara kama kahawa, ndizi, majani ya chai na upandaji miti hasa ya mbao.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.