From Wikipedia, the free encyclopedia
Buhangaza ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35538 [1].
Kijiografia imezungukwa na mto maarufu kwa jina la mto Ngono na milima ya ikunjo.
Kata hiyo inaundwa na vijiji vinne ambavyo ni: Buyaga, Buhangaza, Kashenge na Rwenshato.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 6,350 [2].Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,603 waishio humo.[3]
Kata hii ina jumla ya shule tatu za msingi ambazo ni pamoja na Buhangaza, Rwenshato na Buyaga, pia ina shule moja ya sekondari ya Ikondo.
Katika kata hii shughuli kuu za kiuchumi ni pamoja na kilimo cha zao la kahawa pamoja na migomba. Shughuli nyingine ndogondogo zinazofanyika katika kata hii pamoja na kilimo, ni biashara, uvuvi na ufugaji.
Chakula cha asili, kama ilivyo kwa mkoa wote wa Kagera, ni ndizi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.