Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
"Bernadeta" (Marie-Bernarde) Soubirous (Lourdes, Hautes-Pyrénées, 7 Januari 1844 - Nevers, Nièvre, 16 Aprili 1879) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki nchini Ufaransa.
Tarehe 14 Juni 1925 Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri[1] na tarehe 8 Desemba 1933 mwenyewe alimtangaza mtakatifu bikira.[2]
Sikukuu yake imepangwa tarehe ya kifo chake[3] au 18 Februari, siku ambapo Bikira Maria alimuahidia kumpatia heri, ingawa si katika maisha ya duniani.
Mtoto wa familia fukara sana, anajulikana hasa kwa njozi za Bikira Maria alizojaliwa kwenye pango la Massabielle kati ya tarehe 11 Februari na 16 Julai 1858, akiwa na umri wa miaka 14. Hatimaye Maria alijitambulisha kama Kukingiwa Dhambi ya Asili, sifa yake iliyotangazwa na Papa Pius IX kuwa dogma ya imani Katoliki miaka 4 ya nyuma.[4]
Ingawa viongozi wa Kanisa walikuwa na shaka kwanza, utafiti uliwafanya wakubali ukweli wa tukio hata inaanzishwa adhimisho la Bikira Maria wa Lourdes na patakatifu palipojengwa mahali pake pamekuwa mahali pa hija panapofikiwa na watu zaidi ya milioni 5 kwa mwaka.[5]
Baada ya kujiunga na utawa na kustahimili kwa unyenyekevu matatizo mengi upande wa mwili (kipindupindu, pumu kali, kifua kikuu n.k.) na wa nafsi (dhuluma kutoka kwa watu wasioamini njozi zake au waliomuonea kijicho kwa hizo), alifariki akiwa na umri wa miaka 35 tu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.