From Wikipedia, the free encyclopedia
Apiani wa Kaisarea (Lycia, leo nchini Uturuki, 287 hivi - Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 305 hivi) alikuwa kijana msomi ambaye aliongokea Ukristo.
Kwa sababu ya imani yake, alijaribu kuzuia ibada ya Kipagani, ambayo Wakristo walilazimishwa kuishiriki katika dhuluma ya kaisari Masimino Daia: alimkaribia kishujaa gavana Urbano na kumshika mkono. Hapo akachomwa moto miguu na kutoswa na askari baharini [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.