Kaisarea Baharini
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kaisarea Baharini (kwa Kigiriki Παράλιος Καισάρεια, Parálios Kaisáreia) ulikuwa mji wa Palestina kuanzia mwaka 10 KK hadi 1265 BK.
Kwa sasa ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa la Israeli katika bonde la Sharon[1].
Ulianzishwa na mfalme Herode Mkuu ukawa makao ya liwali wa Dola la Roma aliyetawala Palestina.
Baadaye ukawa kituo muhimu cha Ukristo, ambapo Mtume Petro alibatiza akida Korneli na familia yake (Mdo 10:1-11:18).
Ndipo alipoishi Filipo mwinjilisti (Mdo 8:40) ambaye alimkaribisha Mtume Paulo kwa siku kadhaa (Mdo 21:8-10) katika moja ya nafasi yake ya kupitia mjini huko (Mdo 9:30; 18:22).
Baadaye Paulo alikaa gerezani huko kwa zaidi ya miaka miwili akisubiri kuhukumiwa, mpaka alipokata rufaa kwa Kaisari Nero (23:23; 15:1-13).
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.