From Wikipedia, the free encyclopedia
Akida Korneli (kwa Kigiriki, Κορνήλιος, Kornelios) alikuwa akida wa kikosi cha Italia katika jeshi la Dola la Roma aliyefanya kazi huko Kaisarea Baharini (Palestina). Huko alivutiwa na dini ya Uyahudi hata akajitolea kujenga sinagogi, pamoja na kusali.
Wongofu wake na wa jamaa zake unasimuliwa mara tatu na Matendo ya Mitume kwa jinsi ulivyotiwa maanani na Luka mwinjili aliyetaka kueleza kwamba desturi ya kubatiza watu wa mataifa bila kudai kwanza watahiriwe ilianzisha na Mtume Petro kwa kuangazwa na Mungu (Mdo 10).
Suala hilo lilisumbua sana Kanisa la mwanzo hata baada ya Mtaguso wa Yerusalemu (49 BK) kupitisha desturi hiyo (Mdo 15).
Baada ya kuongoka, inasimuliwa kwamba alishuhudia Injili hadi Misia (leo nchini Uturuki) akateswa kwa ajili hiyo.
Habari nyingine zinasema alipata kuwa askofu na nyingine alifia dini, lakini hazisadikiki sana [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Oktoba[2][3] lakini pia 13 Septemba au 2 Februari.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.