Anemia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Anemia (kutoka Kiingereza; katika lugha hiyo inaandikwa pia anaemia) ni ugonjwa wa kukosa idadi ya kutosha ya seli nyekundu za damu (upungufu wa hemoglobini katika damu).[1][2]

Ukweli wa haraka Matamshi, Kundi Maalumu ...
Anemia
Mwainisho na taarifa za nje
Matamshi
  • Kosa la hati: Hakuna moduli kama "IPAc-en".
Kundi MaalumuHematology 
ICD-10D50.-D64.
ICD-9280-285
DiseasesDB663
MedlinePlus000560
eMedicinemed/132 emerg/808 emerg/734
MeSHD000740
Funga

Kwa lugha nyingine, anemia ni uwezo mdogo wa damu kusafirisha oksijeni mwilini.[3]

Kama anemia inaanza polepole dalili zake mara nyingi ni dhaifu, zikiwa pamoja na uchovu, udhaifu na ugumu wa kupumua.

Anemia inayoanza ghafla ina dalili kali zaidi, zikiwa pamoja na kuchanganyikiwa akilini, kujisikia kama karibu na kupotea, ufahamu au kupotea ufahamu kweli, au kiuu kikali. Kama anemia imeendelea watu weupeweupe wanaweza kuonekana weupe zaidi kuliko kawaida; Waafrika mara nyingi huonyesha rangi ya njano chini ya kucha. Additional symptoms may occur depending on the underlying cause.[4]

Aina za anemia

Kuna hasa aina 3 za anemia

  • Kutokana na upotevu wa damu
  • kutokana na upungufu wa uzalishaji wa seli nyekundu za damu mwilini
  • kutokana na uharibifu wa seli nyekundu katika damu.

Sababu za upotevu wa damu ni pamoja na jeraha, hasa jeraha ndani ya utumbo.

Sababu za upungufu wa uzalishaji wa seli nyekundu ni uhaba wa chuma, uhaba wa vitamini B12 na matatizo ndani ya uboho wa mifupa unaozalisha seli hizi.

Uharibifu wa seli nyekundu za damu husababishwa na anemia selimundu, magonjwa kama malaria na mengine

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.