From Wikipedia, the free encyclopedia
Seli nyekundu za damu (pia erithrosaiti , kutoka Kiingereza red blood cells au erythrocyte) ni seli za damu zenye rangi nyekundu.
Kazi yake ni hasa kubeba oksijeni kutoka mapafu kwenda mwilini mwote.[1][2] Seli nyekundu za damu hupokea oksijeni katika mapafu na kuachana nayo wakati zinabanwa katika mishipa ya damu midogo mwilini.
Rangi nyekundu inatokana na protini ya hemoglobini ndani yake.
Damu ya wanawake huwa na seli nyekundu milioni 4.8 kwa mikrolita ya damu. Damu ya wanaume huwa na seli milioni 5.4 kwa ml.[3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.