Yohane wa Beverley
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane wa Beverley (Harpham, karne ya 7 – Beverley, 7 Mei 721) alikuwa mmonaki Mbenedikto, halafu askofu wa Hexham, na hatimaye askofu mkuu wa York, Uingereza (705-717/718) hadi alipong'atuka arudi kama abati katika monasteri aliyoianzisha.
Sifa zake zimeandikwa na Beda, aliyepewa naye ushemasi na upadri, akithibitisha kwamba daima aliunganisha maisha ya sala na juhudi za kichungaji.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu[1]. Sifa hiyo ilithibitishwa na Papa Benedikto IX mwaka 1037[2].