Yohane Nepomuk Neumann
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yohane Nepomuk Neumann, C.Ss.R. (Prachatice[1], Austria-Hungaria [2], 28 Machi 1811 ā Philadelphia, Marekani, 5 Januari 1860) alikuwa Mkristo wa Bohemia (Ucheki) aliyehamia Marekani mwaka 1836 ili aweze kupata upadrisho[3], akapewa baada ya wiki tatu tu.
Halafu akajiunga na Waredentori ili kufaidika na maisha ya kijumuia (1840)[4] na hatimaye akawa askofu mkuu wa Philadelphia (1852ā1860). Katika jimbo kuu hilo aliunda mfumo wa shule wa kijimbo wa kwanza nchini Marekani: chini yake kutoka 1 tu, shule zake zikawa 200. Pamoja na kushughulikia sana malezi ya watoto, aliwajibika kwa hali na mali kwa ajili ya umati wa wahamiaji fukara[5].
Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Oktoba 1963 na mtakatifu tarehe 19 Juni 1977[6] , mwanamume wa kwanza (na hadi sasa wa pekee) raia wa nchi hiyo[7].