![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/a2/Tanzania_Rombo_location_map.svg/langsw-640px-Tanzania_Rombo_location_map.svg.png&w=640&q=50)
Wilaya ya Rombo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Wilaya ya Rombo ni miongoni mwa wilaya saba za mkoa wa Kilimanjaro upande wa mashariki wa mlima.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/a2/Tanzania_Rombo_location_map.svg/250px-Tanzania_Rombo_location_map.svg.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/33/Rombo_mjini_2006.jpg/640px-Rombo_mjini_2006.jpg)
Makao makuu ya wilaya hiyo yanapatikana katika mji mdogo wa Mkuu, kata ya Kelamfua Mokala. Wenyeji ni hasa Warombo.
Wilaya imepakana na Kenya upande wa kaskazini na mashariki, wilaya ya Hai upande wa magharibi na wilaya ya Moshi vijijini upande wa Kusini.
Idadi ya wakazi ilikuwa 260,963 wakati wa sensa ya mwaka 2012. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 275,314 [1].