From Wikipedia, the free encyclopedia
Wilaya ya Missenyi ni kati ya wilaya 8 za Mkoa wa Kagera, yenye postikodi namba 35300 [1]. Ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Bukoba.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 202,632 [2] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 245,394 [3].
Wilaya hii imepakana na Uganda upande wa kaskazini, Ziwa Viktoria upande wa mashariki na Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera upande wa kusini.
Eneo la wilaya ni km² 2709 na liko upande wa magharibi ya Ziwa Viktoria. .
Maeneo ya wilaya hupokea mvua mara mbili kwa mwaka; kwenye mwambao wa Ziwa Viktoria mvua hufikia hadi milimita 1,400 na 2,000 kwa mwaka, kwenye nyanda za juu kati ya mm 1,000 na 1,400; upande wa magharibi kiwango hushuka hadi mm 600 na 1,000 kwa mwaka.
Barabara ya lami T4 kutoka Mwanza inapita Missenyi ikielekea Uganda. Barabara ya vumbi T38 inaanza kwenye T4 pale Kyaka ikielekea Wilaya ya Ngara, kupitia Wilaya ya Karagwe.[4]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.