From Wikipedia, the free encyclopedia
Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania na pia ni Jiji.
Jiji la Dodoma | |
Majiranukta: 6°10′23″S 35°44′31″E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mkoa wa Dodoma |
Halmashauri | Halmashauri ya jiji la Dodoma |
Kata | 41 |
Mitaa | 222 |
Serikali[1] | |
- Aina ya serikali | Halmashauri ya jiji |
- Mstahiki Meya | Davis G. Mwamfupe |
- Mkurugenzi wa Jiji | Joseph C. Mafuru |
Idadi ya wakazi (2022)https://www.nbs.go.tz | |
- Wakazi kwa ujumla | 765,179 |
EAT | (UTC+3) |
Msimbo wa posta | 411xx |
Kodi ya simu | 026 |
Tovuti: Halmashauri ya Jiji la Dodoma |
Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973, lakini mnamo tarehe 26 Aprili 2018 katika maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano John Magufuli aliupandisha hadhi na kutangaza rasmi kuwa Dodoma ni Jiji.[2][3] [4][5][6] Ofisi kuu za wizara na taasisi nyingi za serikali hatimaye zilihamia Dodoma katika miaka 2016 - 2019.[7][8]
Jiji hili pia ni makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na eneo lake linahesabiwa kama Wilaya ya Dodoma yenye postikodi namba 41100[9].
Eneo la mji liko mita 1135 juu ya usawa wa bahari UB. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji wa Dodoma ulikuwa na wakazi wapatao 410,956 waishio humo.[10]: 17 Mwaka 2022 walihesabiwa 765,179 [11].
Neno "Dodoma" linasemekana kumetokana na neno la Kigogo "dodomia" kufuatilia historia kwamba zamani kuna tembo alikuja pale mjini akakita nyayo zake ardhini akiacha alama ya nyayo zake zimedidimia.
Dodoma ilianzishwa mwaka 1910[12] wakati wa ukoloni wa Kijerumani kama kituo kwenye reli ya kati penye karahana ya reli. Tangu mwaka 1912 imekuwa makao makuu ya Mkoa wa Dodoma wa D.O.A..
Mwaka 1913 Dodoma ilikuwa na posta, simu, hoteli na maduka 26 (moja ya Mzungu, mengine ya Wahindi na Waarabu). Kikosi cha polisi kilikuwa na askari 59.
Dodoma imeendelea kuwa mji mdogo mpaka kutangazwa kuwa mji mkuu. Azimio hili lilileta ujenzi wa maofisi kadhaa ya serikali.
Kwa ujumla uhamisho ulichelewa kwa sababu mbalimbali; sababu muhimu ni ya kwamba watumishi wa serikali na wanasiasa walio wengi hawakupenda kuondoka katika jiji halisi na kuhamia mji ambao ni mbali sana na mazingira waliyoyazoea. Pia matatizo ya kifedha yalisaidia kutangaza nia ya kuhamia lakini kubaki palepale.
Hali halisi bunge lilikuwa linakutana Dodoma lakini makao ya kikazi ya serikali ya Tanzania yalibaki Dar Es Salaam pamoja na ikulu ya rais hadi mwaka 2016. Ndipo kwa amri ya rais mpya, John Magufuli, sehemu kubwa ya ofisi za wizara zimepelekwa Dodoma. Ofisi nyingi zimejengwa katika kata ya Mtumba, takriban kilomita 30 utoka kitovu cha jiji[13].
Kiuchumi ni kitovu cha kilimo na biashara ya karanga, maharagwe, alizeti na mizabibu, pamoja na mifugo na kuku. Pia Dodoma ni mji unaosifika kwa ulimaji wa zabibu na uvunaji wa ubuyu.
Elimu inahitaji kuboreshwa, hasa maeneo ya vijijini, maana ndio mji mkuu: hivyo kunahitajika kuboreshwe zaidi.
Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Dar Es Salaam, pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo na barabara ya kale ya "Cape Town - Cairo" inayopitia Dodoma kutoka kaskazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini (Iringa). Barabara nyingine ni za udongo tu.
Kuna pia njia ya reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara.
Dodoma ina uwanja wa ndege wa kitaifa na vyuo vikuu, kikiwemo kile kikubwa zaidi Afrika Mashariki.
Dodoma kuna makao makuu ya Kanisa la Biblia Publishers pamoja na Emmaus Shule ya Biblia.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.