Waziri Mkuu wa Tanzania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Waziri Mkuu wa Tanzania ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.[1] Anateuliwa na rais akihitaji kuthebitishwa na wabunge wengi.[2]
Waziri Mkuu si kiongozi wa serikali lakini anaongoza vikao vya baraza la mawaziri wakati rais na makamu wa rais hawapo.[3]