From Wikipedia, the free encyclopedia
Wasani (au Wakhoisan kutoka Kiingereza: Khoisan /ˈkɔɪsɑːn/, au Khoe-Sān, tamka [kxʰoesaːn], kulingana na othografia ya kisasa ya Khoekhoegowab) ni kundi la makabila ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambayo ndio wakazi asili wa maeneo hayo, na ambayo yanachanga sura na lugha kwa kiasi kikubwa, tofauti na Wabantu ambao siku hizi ndio wakazi wake walio wengi.[3]
Wasani wengi ndio wazao wa moja kwa moja wa mtawanyiko wa mapema sana wa wanadamu wa kisasa hadi Kusini mwa Afrika kabla ya miaka 150,000 iliyopita ambapo walifika katika Zama za Mwanzo za Mawe.[4] Wengi wao zaidi walimezwa na makabila ya Kibantu, kwa mfano Watswana na Waxhosa.
Nchini Tanzania, waliobaki wa jamii hiyo wanaitwa Wasandawe.
Huko Kusini mwa Afrika wanaishi hasa Namibia (ambapo Wakhoekhoe wa makabila ya Wanama na Wadamara ni makabila yaliyoenea), Botswana na Afrika Kusini, lakini pia Angola, Zambia, Zimbabwe, Lesotho. Baadhi ("San", kwa Kiingereza Bushmen; neno San linatokana na lugha ya Khoekhoe likimaanisha "wale wanaookota vitu kutoka ardhini", yaani ambao hawamiliki mifugo. Ingawa kuna kosmologia na lugha zinazohusishwa na mtindo huu wa maisha, neno hili ni kiwakilishi cha kiuchumi badala ya kitamaduni au kikabila) wamedumisha zaidi taratibu za utamaduni wao kama wawindaji-wakusanyaji, baadhi ("Khoi", yaani "watu", kwa Kiingereza Hottentots) wameiga ufugaji wa makabila ya Kikushi na ya Kibantu yaliyovamia maeneo yao si zaidi ya miaka 3,000 iliyopita, takriban kati ya miaka 1,500 na 2,000 iliyopita.
Machotara wengi wa leo Kusini mwa Afrika wana asili ya baba Mzungu na mama Khoi.
Lugha zao leo zimegawanyika katika angalau familia tatu za lugha tofauti na zisizohusiana: Khoe-Kwadi, Tuu na Kxʼa.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.