Wanawake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahara ni wanawake ambao walizaliwa, wanaishi au wanatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahara katika eneo la Sahara ya Magharibi au makambi ya wakimbizi ya Sahrawi. Katika jamii ya Sahrawi wanawake wanashiriki katika majukumu na kazi mbalimbali ya kijamii pamoja na mashirika Ya kijamii.[1] Kifungu cha 41 cha Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu Kinahakikisha kwamba serikali itazingatia kukuza ushiriki wa wanawake katika masuala ya kisiasa, kijamii na kitamaduni kwa ajili ya maendeleo na ukuaji wa taifa.
Mavazi yanayovaliwa na wanawake wa Sahrawi ni pamoja na vazi linaloitwa Daraa na kitambaa cha kichwani kinachojulikana kama Mefhla.[2][3]
Katika uchaguzi wa mwaka 2012 katika bunge la Sahrawi, asilimia 35 ya wabunge walikuwa wanawake na katika uchaguzi wa mwaka 2008, wanawake walipata walifanikiwa kupata asilimia 34.61 ya viti vya uwakilishi bungeni.[4]
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.