From Wikipedia, the free encyclopedia
Wamuwahidun (kwa Kiing.: Almohad kutoka Kiarabu: al-muwahhidun, yaani "Wanaomwamini Mungu mmoja") walikuwa nasaba ya Waberberi Waislamu waliotawala Afrika ya Kaskazini kutoka bahari Atlantiki hadi Libya pamoja na Al-Andalus yaani kusini mwa Hispania.
Wamuwahidun walianza kama kundi la wafuasi wa Ibn Tumart aliyekuwa mtaalamu wa Kiislamu na mhubiri kutoka Waberberi wa Moroko kusini. Katika mahubiri yake alikosoa yale aliyoyaona kama makosa na dhambi ya Waislamu katika himaya ya Wamurabitun; baada ya kufukuzwa mara kadhaa katika miji yao hatimaye mwaka 1121 alitangaza ufunuo wa wito wake kuwa mahdi. Tangu mwaka uliofuata aliongoza mashambulio dhidi ya jeshi na wawakilishi wa watawala Wamurabitun. Mwaka 1130 alijaribu kushambulia mji mkuu Marakesh lakini alishindwa akafa miezi michache baadaye.
Nafasi yake ilichukuliwa na Abd al-Mu'min al-Kumi. Kuanzia mwaka 1130 hadi kifo chake mnamo 1163, Abd al-Mu'min al-Kumi kutoka kabila la Waberberi Masmuda, alishinda watawala wa Almurabitun (Almoravid) na kuwa mtawala juu ya Afrika kaskazini yote hadi Libya. Alikuwa Amiri wa Marakesh mnamo 1149 akavamia na kutwaa Al-Andalus yaani sehemu ya kusini ya Hispania iliyokaliwa na Waislamu wengi wakati ule.
Makhalifa wa kwanza wa Wamuwahidun walionyesha ukali dhidi ya raia wasio Waislamu. Wayahudi na Wakristo walipewa miezi saba halafu kuamriwa kugeukia Uislamu[1]. Wayahudi na Wakristo walipata hivyo kuwa na mashahidi walioamua kutoacha ungamo lao badala ya kusilimu. Upande wa Wakristo mashahidi wafuatao wanakumbukwa katika enzi ya Wamuwahidun:
Mnamo 1170 Wamuwahidun walihamishia mji mkuu wao kwenda Sevilla. Lakini kufikia mwaka 1212 Muhammad III, "al-Nasir" (1199-1214) alishindwa na muungano wa wafalme wanne wa Kikristo wa Kastilia, Aragon, Navarra na Ureno. Wamuwahidun walipoteza karibu maeneo yote ya Kiislamu huko Iberia.
Miji mikubwa ya Cordoba na Sevilla ilianguka katika mikono ya Wakristo katika nusu ya kwanza ya karne ya 13.
Wamuwahidun waliendelea kutawala Afrika kwa muda, lakini walipoteza sehemu kubwa ya eneo lao. Mtawala wa mwisho wa nasaba hiyo, Idris II, alikuwa amebaki na Marakesh pekee. Huko aliuawa na mtumwa mnamo 1269.
Chini ya Wamuwahidun usanifu wa Kiislamu uliona maendeleo makubwa katika ujenzi wa misikiti, madrasa, vyuo, nyumba na majengo mengine. Mbinu mbalimbali za kupamba majengo zilibuniwa zinazoendelea hadi leo katika usanifu wa Moroko.
Waandishi wa Usufii:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.