Wafiadini wa Mar Saba (20 Machi)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Wafiadini wa Mar Saba (20 Machi) (walifia dini katika monasteri ya Mar Saba, leo nchini Palestina, 797) walikuwa wamonaki Wakristo 20 waliouawa na Waislamu kwa ajili ya imani yao.
Walikufa kwa kukosa hewa kutokana na moshi wa moto uliowashwa katika kanisa la Mama wa Mungu.
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.