Uwanja wa michezo Borg El Arab
Uwanja wa mpira wa miguu / From Wikipedia, the free encyclopedia
Uwanja wa Borg El Arab, mara nyingine hufahamika pia kama Uwanja wa Jeshi la Misri au Uwanja wa El Geish- Alexandria, ni uwanja uliozinduliwa mwaka 2005 katika hoteli ya Mediterranean ambayo ni sehemu ya Borg El Arab; tarkibani kilometa 25 magharibi mwa mji wa Alexandria, Misri. Uwanja huu ndio mkubwa zaidi nchini Misri na ni wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya uwanja wa FNB wa jijini Johannesburg), ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 86,000[1] na wote wakiwa wamekaa katika viti. Pia ni uwanja wa 27 kwa ukubwa duniani kwote. Uwanja huu upo jijini Cairo katika eneo la makutano ya barabara ndani ya jangwa la Alexandria takribani kilometa 10 kutoka uwanja wa ndege wa Borg El Arab na kilometa 15 kutoka katikati ya mji wa Alexandria. Kuna njia kwa ajili ya michezo ya mbio kuzunguka eneo la kuchezea la uwanja huo, na kuna minara ya taa katika kila pembe ya uwanja. Jukwaa moja pekee ndilo lililoezekwa.
Uwanja mzima una ukubwa wa mita za mraba 609,000 na kuna ukuta uliozunguka wenye urefu wa kilometa 3 na miundombinu ya barabara yenye urefu wa kilometa 6, eneo la kuegesha magari lenye uwezo wa kuingiza magari 5000 na mabasi 200 kuachana na eneo maalumu kwa ajili ya ndege, pia kuna mageti 136 ya kuingilia. Jukwaa kuu limefunikwa na mwamvuli ambao umefunika tarkibani 35% ya uwanja wote, na ndio mwamvuli mkubwa kuliko yote katika mashariki ya kati. Una urefu wa mita 200 na upana wa mita 60 na eneo la mita za mraba 12,000.
Uwanja huo una mfumo wa hewa katika vyumba vya kubadilishia nguo, saluni na maeneo ya kuingilia, uwanja huo pia una mashine za kupandisha watangazaji na watu muhimu katika majukwaa ya juu ya uwanja. Kuna viwanja viwili vya mazoezi ambavyo vina uwezo wa kuingiza watazamaji 2000, vyumba viwili vya kubadili nguo na eneo kwa ajili ya michezo ya riadha. Uwanja huo una hoteli yenye uwezo wa kuingiza wageni 200 yenye mfumo wa usambazaji hewa pamoja na bwawa la kuogelea, eneo la kufanyia mazoezi na nyumba za idara zenye watu 80. Uwanja huu pia una jengo la mikutano na waandishi wa Habari. Ikijumuisha maeneo ya warusha Habari, viingilio vya dharura, magari ya huduma ya kwanza, maeneo ya kujipatia chakula 39, vyumba vya kujisaidia 337 vinavyojumuisha vyumba 33 kwa ajili ya wanawake na 8 kwa wasiojiweza.