From Wikipedia, the free encyclopedia
Usiku wa Pasaka ni kesha kuu la mwaka wa Kanisa ambapo Wakristo wanashangilia ufufuko wa Yesu katika giza la kati ya Jumamosi kuu na Jumapili ya Pasaka: ndipo Injili zote zinaposimulia kwamba Yesu Kristo aliweza kufufuka baada ya kusulubiwa na kuzikwa siku ya Ijumaa kuu.
Mwaka wa liturujia |
---|
Magharibi |
Mashariki |
Ndio wakati mwafaka wa kubatiza hasa watu wazima, kwa sababu sakramenti hiyo, pamoja na kipaimara na ekaristi, inashirikisha kifo na ufufuko wa Yesu.
Hata hivyo, madhehebu yanatofautiana katika liturujia hata ya sikukuu hiyo.
Kihistoria, usiku wa Pasaka uliadhimishwa na Waisraeli wa kale hasa namna iliyoratibiwa na Torati, ambamo jambo muhimu zaidi ni kula nyama ya mwanakondoo aliyechinjwa kama kafara. Tangu wakati wa Musa mlo huo umekuwa ukumbusho wa kutoka kwao katika unyanyasaji au utumwa nchini Misri.
Yesu alikamilisha hata ibada hiyo kwa kujifanya Mwanakondoo wa Mungu kama alivyotambulishwa na Yohane Mbatizaji katika mto Yordani.
Kwa kujitoa kufa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu na ondoleo la dhambi alivuka kutoka dunia hii kurudi kwa Baba na kuwezesha wote kuacha utumwa wa shetani, dhambi na kifo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.