Unene wa kupindukia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Unene wa kupindukia (kwa Kiingereza "obesity" kutokana na neno la Kilatini obesitas, linalomaanisha "gumu, nono au nene” [1]; jina la kisayansi kwa Kilatini ni "adipositas") ni hali mbaya ambapo mafuta ya ziada ya mwili hulimbikizana hadi kiwango kinachoweza kuathiri vikubwa afya, ikipelekea ongezeko la maradhi na kupungua kwa matarajio ya kuishi. [2][3]
Obesity | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Endocrinology ![]() |
ICD-10 | E66. |
ICD-9 | E |
OMIM | 601665 |
DiseasesDB | 9099 |
MedlinePlus | 003101 |
eMedicine | med/1653 |
MeSH | C23.888.144.699.500 |
Kipimo cha mwili kuwa mnene na mzito mno ni uwiano kati ya urefu wa mtu na uzito wake. Watu hutajika kuwa na unene wa kupindukia wakati nambapeo ya mata ya mwili (NMM), kipimo kinachopatikana kwa kugawanya uzito wa mtu kwa kilogramu kwa mraba wa urefu wake katika mita, kimezidi 30 kg/m2.[4]
Kuwa mneme mno kunaleta hatari ningi kwa afya na kusababisha au kuongeza uwezekano wa magonjwa kama vile:
- Shinikizo la juu la damu
- Ugonjwa wa kisukari
- Maradhi ya moyo
- Ugonjwa wa kupooza
- Shida za kupumua na pumu[5][3]
- Matatizo ya viungo vya miguu na ya uti wa mgongo
- Maradhi ya mishipa,
- Apnea pingani ya usingizi
- Osteoathritisi[3].
Watu wakinenepa mno hufa mapema na kuwa na magonjwa mengi kuliko watu wembamba wanaokula kiasi tu, jinsi wanavyohitaji chakula. Tatizo la unene duniani hukumba wanaume zaidi ya wanawake.
Unene wa kupindukia mara nyingi husababishwa na ujumuisho wa kula chakula kilicho na nguvu nyingi, ukosefu wa mazoezi ya mwili, na urithi wa jeni maalumu, ingawa visa vichache vina msingi wa jeni, matatizo ya kiendrosini, matibabu au maradhi ya akili.
Ushahidi wa kuthibitisha dhana kuwa baadhi ya watu hunenepa ingawa hula kiasi kidogo hautoshi; kwa wastani, watu wanene hutumia nguvu nyingi kuliko watu wenye mwili mdogo kwa sababu ya nguvu zinazohitajika kuimarisha mata kubwa ya mwili.[6][7]
Chakula bora na mazoezi ya mwili ndiyo njia kuu za kutibu unene wa kupindukia. Ubora wa chakula unaweza kuimarishwa kwa kutumia vyakula vilivyo na nguvu nyingi, kama vile vyakula vilivyo na kiwango cha juu cha mafuta na sukari, na kwa kutumia unyuzi wa chakula kwa wingi zaidi.
Dawa za kukabiliana na unene zinaweza kutumiwa kupunguza hamu ya chakula au kuzuia ufyonzaji wa mafuta, huku mtu akila chakula kinachofaa. Iwapo chakula bora, mazoezi na matibabu hayatoshi, mpira wa utumboni unaweza kusaidia kupunguza uzito wa mwili, au upasuaji unaweza kufanywa ili kupunguza ukubwa na/au urefu wa matumbo. Upasuaji huo hupelekea mtu kushiba upesi na kupunguza uwezo wa kufyonza virutubishi vilivyomo katika chakula.[8][9]
Unene wa kupindukia ni kisababishi kinachozuilika cha kifo kilicho kikuu ulimwenguni kote, huku kiwango chake cha ueneaji kikiongezeka kwa watu wazima na watoto. Viongozi huamini kuwa hili ni mojawapo ya matatizo makuu zaidi ya afya ya umma katika karne ya 21.[10]
Unene wa kupindukia hufedheheshwa katika sehemu nyingi za ulimwengu wa kisasa (hasa katika Ustaarabu wa Magharibi[11]), ingawa hali hii ilitazamwa na watu wengi kama ishara ya utajiri na afya bora katika nyakati za awali za historia, na pia huonekana hivyo katika baadhi ya sehemu za dunia.[3][12]