Ukoma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ukoma (pia ugonjwa wa Hansen; kwa Kiingereza: leprosy) ni ugonjwa wa kuambukiza wa kudumu unaosababishwa na bakteria Mycobacterium leprae na M. lepromatosis [1] [2].
Ukoma | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Infectious disease |
ICD-10 | A30. |
ICD-9 | 030 |
OMIM | 246300 |
DiseasesDB | 8478 |
MedlinePlus | 001347 |
eMedicine | med/1281 derm/223 neuro/187 |
MeSH | D007918 |
Baada ya ambukizo kuna kipindi ambapo mgonjwa hana dalili za ukoma. Kipindi hicho bila dalili kinaweza kuendelea hadi miaka 5 au hata miaka 20[2]. Dalili zinazoonekana ni kwa mfano vidonge vya chembe vya neva, vya mfumo wa upumuaji, vya ngozi na vya macho [2].
Wakati dalili zinapoanza kuonekana mgonjwa hasikii tena baridi, joto wala maumivu. Kwa hiyo hatambui kirahisi kama amepata jeraha. Vidonda vinavyotokea haviumi na uchafu pamoja na bakteria hatari zinaingia mwilini. Hivyo vidonda vinaweza kuwa vikubwa zaidi kwa sababu havitibiwi au vinachelewa kutibiwa. Ndiyo sababu pengine wakoma wanapotea viungo vya mwili kama vidole na hata mguu au mkono kutokana na majeruhi yanayorudiarudia.[3]
Udhaifu pamoja na macho kutoona vyema pia yanamwathiri mgonjwa.[3]