![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b5/Saint_Triphyllius.jpg/640px-Saint_Triphyllius.jpg&w=640&q=50)
Trifilo wa Nikosia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Trifilo wa Nikosia (Roma, Italia, au Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, mwanzoni mwa karne ya 4 – Nikosia, Kupro, 370) alikuwa askofu wa mji huo[1].
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/b5/Saint_Triphyllius.jpg/320px-Saint_Triphyllius.jpg)
Baada ya kusoma sheria huko Beirut, Lebanoni[2], aliongokea Ukristo kwa msaada wa Spiridoni wa Tremetusia akasaidia sana kutetea imani sahihi na kupinga teolojia ya akina Ario. Kwa hiyo Atanasi alimsifu.
Maandishi yake [3] yamepotea. Imebaki tu kumbukumbu ya ufasaha wake katika kuhubiri ambao kadiri ya Jeromu ulizidi ule wa wengine wote wa wakati ule[4][5][6][7].
Tangu kale anaheshimiwa na Ukristo wa Mashariki na Ukristo wa Magharibi kama mtakatifu.