Nikosia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nikosia (Kigiriki: Λευκωσία lefkosia; Kituruki: Lefkoşa) ni mji mkuu wa Kupro pia mji mkubwa wa nchi.
Mji umegawiwa tangu vita ya 1974 kuna sehemu ya kigiriki upande wa kusini yenye wakazi 270,000 na sehemu ya kituruki upande wa kaskazini yenye wakazi 80,000. Mpaka hulindwa na wanajeshi wa UM. Kusini ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kupro inayotawaliwa na Wakupro Wagiriki na kutambuliwa kimataifa; upande wa kaskazini ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini nchi isiyotambuliwa kimataifa.
Uwanja wa ndege umefungwa tangu 1979 uko ndani ya eneo linalotawaliwa na UM pekee.