![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/dd/Titan_Visible.jpg/640px-Titan_Visible.jpg&w=640&q=50)
Titani (mwezi)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Titani (kutoka Kigiriki: Τῑτάν)[1] ni mmojawapo kati ya miezi ya sayari Zohali wenye ukubwa wa sayari ndogo. Kipenyo chake kwenye ikweta ni kilomita 5,150[2][3][4] na inasogea kwenye mzingo wenye umbali wa kilomita 1,221,865 km kutoka Zohali. [2] Titani ilitambuliwa mwaka 1655 na mwanaastronomia Christiaan Huygens kwa kutumia moja ya darubini za kwanza iliyoboreshwa. Titani ni mwezi mkubwa wa Zohali na mwezi mkubwa wa pili katika mfumo wa Jua letu. Hata ni kubwa kuliko sayari Utaridi.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/d/dd/Titan_Visible.jpg/320px-Titan_Visible.jpg)