![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/f/f7/Jewel_of_the_Solar_System.jpg/640px-Jewel_of_the_Solar_System.jpg&w=640&q=50)
Zohali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lua error in package.lua at line 80: module 'Module:Navbar/configuration' not found. Zohali ni sayari ya sita kutoka Jua katika Mfumo wa Jua. Ni sayari kubwa ya pili baada ya Mshtarii.
Inaonekana kwa macho matupu si lazima kutumia darubini. Kwa hiyo imeshajulikana tangu zamani ilitambuliwa na wataalamu wa nyakati za kale.
Uso wa Zohali hauonekani kwa sababu angahewa nzito inafunika kila sehemu. Mada ya angahewa ni hasa hidrojeni. Kutokana na uzito wa angahewa shinikizo ndani yake inaongezeka sana katika vilindi vyake na kusababisha gesi za angahewa kuingia katika hali ya giligili inayobadilika kuwa mango hadi metali ndani zaidi.