![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/88/Stanislaw_Kazimierczyk_painting.jpg/640px-Stanislaw_Kazimierczyk_painting.jpg&w=640&q=50)
Stanislaus Kazimierczyk
From Wikipedia, the free encyclopedia
Stanislaus Kazimierczyk (27 Septemba 1433 - 3 Mei 1489) alikuwa padri kanoni wa Kanisa Katoliki nchini Poland maarufu kwa ibada yake kwa Yesu ekaristi na kwa huruma yake kwa maskini[1][2]. Alijitahidi kuhubiri Neno la Mungu na kuwapa watu huduma za kitubio na uongozi wa kiroho.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/8/88/Stanislaw_Kazimierczyk_painting.jpg/640px-Stanislaw_Kazimierczyk_painting.jpg)
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 18 Aprili 1993. Halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010.