Sofroni wa Yerusalemu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sofroni wa Yerusalemu (Damasko, Syria[1], 560 hivi - Yerusalemu, Israeli/Palestina, 11 Machi 638) alikuwa askofu wa Yerusalemu kuanzia mwaka 634 hadi kifo chake[2][3]. Wakati huo Yerusalemu ulitekwa na Waarabu Waislamu naye alitetea imani na haki za wananchi dhidi ya wavamizi.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/1/1e/Sophronius_of_Jerusalem.jpg)
Kabla ya hapo alikuwa mwanafunzi wa Yohane Mosko akaongozana naye kutembelea monasteri nyingi, akawa mwalimu, halafu mmonaki mwanateolojia aliyetetea vizuri imani sahihi kuhusu Yesu Kristo kuwa na utashi wa kibinadamu chini ya ule wa Kimungu.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.