Siku ya Arafah
From Wikipedia, the free encyclopedia
Siku ya Arafah (kwa Kiarabu يوم عرفة, Yawm ‘Arafah) ni maadhimisho ya Kiislamu yanayofanyika katika siku ya tisa ya mwezi wa Dhu al-Hijjah kwa mujibu wa Kalenda ya Kiislamu.[1] Ni siku ya pili ya kufanya Hijja na mwanzo wa kusherehekewa kwa sikukuu ya Eid el Adha.[2] Katika siku hiyo mahujaji wa Kiislamu huelekea katika eneo la Minna katika Mlima Arafah na tambarare yake katika eneo ambalo Mtume Muhammad alitoa hotuba yake ya mwisho ya kuaga.