Samari (Samarium) ni elementi ya kikemia yenye alama Sm na namba atomia 62, maana yake kuna protoni 62 katika atomu. Ni elementi ya kimetali yenye rangi nyeupe-kifedha inayooksidika hewani. Kwenye mfumo radidia inahesabiwa kati ya lanthanidi.
Samari | |
---|---|
Jina la Elementi | Samari |
Alama | Sm |
Namba atomia | 62 |
Mfululizo safu | Lanthanidi |
Uzani atomia | 150,36 |
Valensi | 2, 8, 18, 24, 8, 2 |
Densiti | 7.52 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | °K 1345 |
Kiwango cha kuchemka | °K 2173 |
Hali maada | mango |
Samari iligunduliwa mnamo 1879 na Mfaransa Paul-Emile Lecoq de Boisbaudran. Ilipokea jina lake kutokana na madini Samarskiti ya madini ambayo ilitengwa. Madini yenyewe ilipata jina lake kwa heshima ya afisa wa migodi wa eneo la Urusi ambako madini yalitambuliwa mara ya kwanza.
Madini hayo hupatikana zaidi nchini Uchina, Marekani, Brazil, India, Sri Lanka na Australia; Uchina unaongoza ulimwenguni katika uchimbaji wa madini ya samari.
Samari haipatikani katika hali safi ila iko ndani ya madini mengi. Akiba za duniani kote za samari zinakadiriwa kuwa tani milioni mbili; Uzalishaji wa kila mwaka ni karibu tani 700. [1] China ina uzalishaji mkubwa zaidi na tani 120,000 zilizochimbwa kwa mwaka; inafuatwa na Marekani (kama tani 5,000) na India (t 2,700). [2] Samari kwa kawaida huuzwa kama oksidi.[3]
Samari ni metali ya ardhi adhimu yenye ugumu na densiti ya kufanana na zinki. Ugumu na wiani sawa na ile ya zinki. Kiwango cha kuchemsha ni °C 1794.
Matumizi ya kibiashara ya samari yapo hasa kwenye sumaku za samari-kobalti ambazo ni sumaku za kudumu. Zina faida ya kuvumilia halijoto hadi nyuzijoto °C 700 bila kupoteza tabia zake za kisumaku.
Isotopi ya samari-149 ina uwezo wa kufyonza nyutroni na kwa hiyo inatumiwa kudhibiti mchakato ndani ya matanuri ya nyuklia.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.