Rosh Hashanah
From Wikipedia, the free encyclopedia
Rosh Hashanah (kwa Kiebrania: רֹאשׁ הַשָּׁנָה, Rōʾš hašŠānā, yaani "mwanzo wa mwaka") ni siku ya kwanza ya mwaka wa Kiyahudi. Ni sikukuu ya kwanza katika mfuatano wa siku takatifu za Uyahudi kwenye mwanzo wa mwaka jinsi zilivyobainishwa na Mambo ya Walawi 23:23–25 [1]. Tarehe yake hutokea kwa kawaida katika mwezi wa Septemba, hadi 5 Oktoba.
Rosh Hashanah ni maadhimisho na sherehe ya siku mbili ambayo huanza siku ya kwanza ya mwezi wa Tishri, ambao ni mwezi wa saba baada ya Pasaka ya Kiyahudi. Hukumbuka uumbaji wa Adamu na Hawa waliokuwa watu wa kwanza kufuatana na taarifa ya Biblia.