Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Petro-Henri Dorie, M.E.P. (Saint-Hilaire-de-Talmont, Vendée, Ufaransa, 23 Septemba 1839 - Sai-Nam-Hte, 7 Machi 1866) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Padri huyo mmisionari alikatwa kichwa pamoja na askofu Simeoni-Fransisko Berneux na mapadri wawili wa shirika lake: Yusto Ranfer na Alois Beaulieu kwa sababu, walipoulizwa na watesi wamefika Korea kufanya nini, walijibu kwa ujasiri na unyofu kwamba wana lengo la kuokoa watu kwa jina la Yesu[1].
Hao na wafiadini wenzao 99 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[2]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba.
Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[3] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[4].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.