Papa Siricius
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Siricius alikuwa Papa kuanzia tarehe 15 au 22 au 29 Desemba 384 hadi kifo chake tarehe 26 Novemba 399[1]. Alitokea Roma, Italia na baba yake aliiitwa Tiburtius.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/7/70/Siricius.jpg)
Alimfuata Papa Damaso I[2] akafuatwa na Papa Anastasius I.
Alikuwa mtendaji na kukabili masuala mbalimbali. Amri zake 15 (hati Directa) kuhusu maisha ya Kanisa ni za kwanza kutufikia nzima bila kasoro.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.