Papa Damaso II
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Damaso II (alifariki 9 Agosti 1048) alikuwa Papa kuanzia tarehe 17 Julai 1048 hadi kifo chake siku chache baadaye[1]. Alitokea Bavaria, Ujerumani, ila alikuwa askofu wa Brixen, leo nchini Italia.
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Poppo.
Alimfuata Papa Benedikto IX akafuatwa na Papa Leo IX.