Nyamatongo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyamatongo ni kata ya Wilaya ya Sengerema katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Msimbo wa posta ni 33334.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 16,414 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 26,707 waishio humo.[2]
Wakazi asili wa kata hiyo ni kabila la Wazinza. Kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji ambao ni Wakara, Wakerewe, Wajita na Wasukuma ambao wanazidi wenyeji kwa idadi.