![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/67/Nakuru_montage.png/640px-Nakuru_montage.png&w=640&q=50)
Nakuru
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nakuru ni mji wa Kenya ambao ni makao makuu ya kaunti ya Nakuru. Ukiwa na wakazi 307,990 (sensa ya 2009) ni mji mkubwa wa nne nchini Kenya baada ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/6/67/Nakuru_montage.png/640px-Nakuru_montage.png)
Nakuru | |
Mahali pa mji wa Nakuru katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°17′0″S 36°04′0″E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Nakuru |
Idadi ya wakazi (2009) | |
- Wakazi kwa ujumla | 307,990 |
Uko kwenye kimo cha m 1860 juu ya UB katika mashariki ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki kando ya ziwa Nakuru.
Mji ulianzishwa na Waingereza mwaka 1904 kwenye njia ya reli ya Uganda. Kiasili eneo lilikuwa makao ya Wamasai waliopaita mahali "en-akuro" yaani mahali pa vumbi. Waingereza waliweka maeneo haya kando hasa kwa walowezi wazungu waliopewa mashamba makubwa. Nakuru ikawa kitovu cha "White Highlands" (Nyanda za juu za watu weupe).
Siku hizi Nakuru bado ni mji muhimu kwa kilimo cha mashamba makubwa yaliyo mkononi mwa tabaka la juu mpya ya Kiafrika tangu uhuru. Watalii wengi kidogo wanafika Nakuru wakitembelea hifadhi ya Nakuru ambayo ni karibu sana na mji mwenyewe.