![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/38/Overview_lakenakuru.jpg/640px-Overview_lakenakuru.jpg&w=640&q=50)
Ziwa Nakuru
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ziwa Nakuru ni mojawapo ya maziwa ya magadi katika Bonde la Ufa. Linapatikana kusini mwa mji wa Nakuru, katika eneo la kati nchini Kenya na linazungukwa na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru. Hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1961. Ilianza ndogo, ikizingira ziwa hilo maarufu na maeneo ya milima yaliyo karibu. Na sasa imeongezwa kujumuisha sehemu kubwa ya maeneo ya mbuga.
Wingi wa mwani katika ziwa hili huvutia kwa kiasi kikubwa ndege aina ya flamingo ambayo hupatikana sana katika ufuo wa ziwa hili.
Ndege wengine pia hustawi katika eneo hili, na hata wanyamapori wakubwa.
Mito inayoingia ziwani ni: mto Enchorro, mto Enderit, mto Isirkon, mto Lamuriak na mmojawapo kati ya mito inayoitwa mto Makalia. Kiwango cha maji katika ziwa hili kilishuka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya 1990 lakini hivi karibuni kimeweza kurejea kiwango cha kale.
Maana ya Nakuru ni "vumbi" au "Mahali pa vumbi" katika lugha ya Kimaasai.
Ziwa Nakuru imelindwa chini ya Mkataba wa Ramsar ya maeneo ya maji.