Nabii Mika, ambaye jina lake la Kiebrania מיכה linamaanisha "Nani kama Mungu?", alifanya kazi wakati mmoja na nabii Isaya (miaka 740-700 hivi K.K.).

Thumb
Nabii Mika kadiri ya Gustave Doré.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 21 Desemba[1] na 14 Agosti, lakini pia 14 Januari, 18 Januari na 31 Julai[2].

Ujumbe

Ujumbe wake unajulikana kupitia kitabu chenye jina lake katika gombo la Manabii Wadogo (Kitabu cha Mika)

Humo tunasoma kwamba yeye, kama vile Isaya, alitetea haki za wanyonge (2:1-11) na kutabiri adhabu.

Lakini hasa alitabiri juu ya Masiya, kwamba atazaliwa Bethlehemu (5:1-3), tunavyosoma katika Injili ya Mathayo kuhusu uzazi wa Yesu Kristo.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.