Mto Kalambo
From Wikipedia, the free encyclopedia
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/ad/Kalambo_Falls.jpg/220px-Kalambo_Falls.jpg)
Mto Kalambo ni mmojawapo kati ya mito ya Tanzania (upande wa kusini magharibi, mkoa wa Rukwa) na ya Zambia (upande wa kaskazini), ukiwa mpaka kati ya nchi hizo mbili kwa sehemu fulani.
Ni maarufu kwa maporomoko yake. Maji yake yanaishia bahari ya Atlantiki kupitia ziwa Tanganyika na mto Kongo.