Maporomoko ya Kalambo
maporomoko ya maji kwenye Mto Kalambo nchini Zambia na Tanzania / From Wikipedia, the free encyclopedia
Maporomoko ya Kalambo yanatokana na mto Kalambo ambao ni mpaka wa Tanzania na Zambia.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/ad/Kalambo_Falls.jpg/250px-Kalambo_Falls.jpg)
Maporomoko ya maji hayo ya mita 235 kwa mkupuo mmoja, ukiachilia kuwa ni ya pili baada ya yale ya Tugela (Afrika ya Kusini), lakini pia ndiyo maporomoko pekee yanayogawa nchi mbili.
Maporomoko hayo yapo katika kijiji cha Kapozwa, kata ya Kisumba, Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa. Katika kijiji cha Kapozwa, ambacho kilianzishwa kutokana na imani kuwa ukienda kuoga katika maporomoko hayo utapooza. Kwa kuambiwa hivyo wenyeji wa eneo hilo walipaita kijiji jina la Kapozwa.
Maporomoko hayo yamekuwa yakionekana na kutangazwa kuwa yapo Zambia na hivyo kuiondoa Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye maporomoko yanayotambulika duniani.